Wednesday, January 15, 2014

FUNGUA www.habarikatavi.wordpress.com

USIPOTEZE MUDA FUNGUA www.habarikatavi.wordpess.com
Katavi

BARAZA la madiwani la Halmashauri ya Mji wa Mpanda Mkoa wa Katavi  limepitisha bajeti ya shilingi Bil 36 katika mapato  yake  ya 2014 na 2015

Kwa mujibu wa ndugu Suleimani Lukanga ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, halmashauri yake inatarajia kujipatia kiasi cha shilingi 36, 229,866,934 katika mwaka wa fedha wa 2014/15.

Lukanga alibainisha  hayo katika kikao  maalumu  cha Baraza  la   Madiwani  kilichofanyika  Jumatano Januari 15, 2014 katika  ukumbi wa  Chuo  Kikuu Huria cha Mkoa wa Katavi mjini Mpanda

Alisema ofisi yake imeandaa Bajeti hiyo kwa kuzingatia mwongozo wa Bajeti ya Taifa ya kuondoa umasikini ambapo kati ya  Fedha  hizo  Sh 8,192, 020,461  ni  mishahara ya watumishi  ruzuku ya kutoka Serikali kuu.

Aidha alisema matumizi  mengine ya fedha za Maendeleo ni  Sh 25,535,581,473 na fedha  za makusanyo ya ndani na makusanyo  ya huduma za afya na  na ada za Sekondari halmashauri hiyo inatarajia kukusana  Sh 1,285,460 

Alisema  pia alimashauri hiyo imeomba  maombi maalumu  nje ya ukomo wa Bajeti  shilingi  3,302 500,000 na kufanya bajeti hiyo kufikia   Sh 39,532,366,934

Alisema Bajeti ya mwaka wa 2013 na 2014  Halmashauri ya mji wa Mpanda iliidhinisha  jumla ya  shilingi  12,833,792,818 lakini hadi kufikia Novemba  2013 Halmashauri ilikuwa imepokea  jumla ya Sh  4,165,656,732 ambazo ni sawa na  asilimia 28  ya Bajeti  iliyoidhinishwa  kwa mwaka wa fedha wa 2013  na 2014-01-15

Aidha  alieleza kuwa  ongezeko hilo la Bajeti  limeongezeka kutokana na ongezeko la  watumishi wa ajira mpya  na ongezeko la miradi ya maendeleo katika kata zote tisa za Halmashauri hiyo  pamoja na huduma mbalimbali

Hata  hivyo Lukanga  alisema  Bajeti ya msimu uliopita ya mapato ya ndani ilikuwa ni  Tsh  Milioni  926,422 wakati msimu wa Fedha wa mwaka huu  mapato ya ndani ni  Tsh Bilioni 1,285,460,000 ambalo ni  sawa la ongezeko la asilimia  38.8  ya Bajeti ya Halmashauri ya msimu uliopita
mwisho

Friday, November 29, 2013

MABORESHO

KUANZIA TAREHE 1, DESEMBA 2013 TUTAKUWA TUNAPATIKANA KATIKA MTANDAO MPYA KUTOKANA NA MABORESHO YANAYOENDANA NA MABADILIKO YA KITEKNOLOJIA NA KULINDA USALAMA NA MAADILI YA KAZI TUNAZOZIWEKA KATIKA MEDIA HII. .....

MTANDAO MPYA WA KUPATA HABARI ZA UHAKIKA ZILIZOFANYIWA UCHUNGUZI WA KINA NI www.habarikatavi.wordpress.com

KATIKA MEDIA HII MPYA UTAPATA NAFASI YA KUTOA MAONI YAKO KWENYE UWANJA TULIOKUWEKEA TUNACHOOMBA NI KUZINGATIA MAADILI NA KUEPUKA USHABIKI WA AINA YOYOTE ILE

KAZI ZOTE ULIZOKUWA UNAZIPATA KATIKA MEDIA HII UTAZIPATA KATIKA MEDIA MPYA

MMILIKI WA MEDIA ANAOMBA RADHI KWA USUMBUFU UTAKAOJITOKEZA
Blogger
Sumia W.
For SMS
0767 51 99 89
Email: willysumia@gmail.com


Sunday, November 17, 2013

TMF YAANZA KUTOA MAFUNZO YA UBORESHAJI WA UANDISHI WA MITANDAO YA KIJAMII NCHINI TANZANIA

ukumbi wa Mvumi
  
BEDA MSIMBE AKIFAFANUA NAMNA MITANDAO INAVYOWEZA KULETA MATATIZO KWA BLOGGER
  
MR SAIMON M. MKINA LECTURING BLOGGERS AT DODOMA HOTEL
on progress class




Leading Crue at Mvumi Hall Dodoma Hotel


 Washiriki  wa mafunzo ya  uboreshaji wa  uandishi wa  mitandao  ya  kijamii kama blog  na mingine  wakiwa katika ukumbi  wa   Dodoma  Hotel  leo  ni mafunzo ya siku  nne  kuanza  leo
 Ma bloga kutoka  mikoa  mbali mbali wakiwa katika darasa  la mafunzo ya uboreshaji uandishi wa mitandao ya kijamii chini ya  ufadhili wa TMF 
 











WEKEZA KATIKA SHULE HII

TITTLE No. 37755 Registered Mwanza
LAND plot No. 122 
BLOCK 'P' low Density
Mbulu Kahama Urban Area
GURANTEE ; 33 yrs
MMILIKI; BERTHA MABULA KINUNGU
SIMU: +255756 01 83 36










KAMA UNAHITAJI WASILIANA NA MMILIKI WA SHULE: Bertha Mabula Kinungu wa S. L. P 34 Kahama; simu No. +255756 01 83 36
Email: willysumia@gmail.com
BEI NI NAFUU SANA

HALMASHAURI ZAAGIZWA KUJENGA MAKTABA ZAO



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema kila Halmashauri hapa nchini inapaswa kuweka kwenye mpango wake wa maendeleo kifungu cha ujenzi wa maktaba ya wilaya ili watu waweze kusoma na kujiendeleza kwa urahisi.
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Jumamosi, Novemba 16, 2013) wakati akiwahutubia washiriki wa mahafali ya 19 ya Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi wa Nyaraka cha Bagamoyo yaliyofanyika kwenye viwanja vya chuo hicho nje kidogo ya mji wa Bagamoyo.
Jumla ya wahitimu 749 walitunukiwa vyeti kati yao 244 vikiwa ni vya stashahada na 505 ni vya astahada katika fani za ukutubi na utunzaji nyaraka.
Alisema ukutubi ni mojawapo ya fani kongwe hapa duniani japo haiongelewi sana hapa nchini. “Hili ni eneo linalomgusa kila mmoja wetu, kuanzia mtu wa kawaida awe mkulima, mvuvi, seremala, mjasiriamali ama yeyote ambaye anahitaji taarifa mbalimbali zimsaidie katika maendeleo yake. Hali kadhalika, mwanafunzi, msomi na mwanataaluma yeyote hawezi kufikia upeo wa masomi na taaluma yake kama hakusoma vitabu na machapisho yaliyoko katika maktaba ambavyo vinatunzwa mkutubi.
Alisema kati ya wilaya 133 zilizopo hapa nchini, ni wilaya 19 tu ambazo zimejenga maktaba katika ngazi ya wilaya. “Hii ni sawa na asilimia 14.2 tu ya wilaya zote. Upungufu huu unasababishwa na tatizo la watu kutotambua umuhimu wa kuwa na maktaba na katika hili lawama ni lazima wabebeshwe Wakurugenzi wa Halmashauri,” alisema.
Waziri Mkuu alisema katika ngazi ya mikoa hali si mbaya kwani mikoa 22 kati ya 25 ya Tanzania Bara ina maktaba za mkoa.
“Tunazo Halmashauri 167 lakini ni Halmashauri 19 tu ambazo zina maktaba... nitoe wito kwa wilaya zote ambazo hazina maktaba zione umuhimu wa kuwa na maktaba zake. Tukifanikiwa kuwa na maktaba katika kila mkoa na kila wilaya itatuwia rahisi kuisogeza huduma hiyo katika ngazi ya kata ili iwe karibu zaidi na wananchi,” alisema.
Akisisitiza umuhimu wa fani hiyo Waziri Mkuu alisema mahitaji ya wakutubi hapa nchini ni makubwa kwani hapa nchini kuna shule za msingi zaidi ya 16,300 na shule za sekondari zaidi ya 4,500 za Serikali na za binafsi.
“Tunawahitaji zaidi hawa wakutubi katika shule zetu kwani wakiwepo kwenye shule zetu watakuwa karibu na wanafunzi na wataweza kuwasaidia wanafunzi kupanua uelewa wao,” alisisitiza.
Aliahidi kufuatilia maombi ya bajeti ya maendeleo ya chuo ili kukisaidia chuo hicho kiwe bora zaidi.
Mapema akitoa taarifa ya chuo hicho, Mkuu wa Chuo hicho, Bw. Zuberi Khatibu alisema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto ya uhaba wa madarasa licha ya kuwa udahili umekuwa ukiongezeka mwaka hadi mwaka.
“Mwaka 2007/2008 chuo kilidahili wanafunzi 100 lakini katika mwaka 2012/2013 tulidahili wanafunzi 708 na mwaka huu wa masomo (2013/2014) tumedahili wanafunzi 821,” alisema.
Naye Mwenyekiti wa Baraza la Chuo hicho, Dk. Alli Mcharazo, alisema kabla chuo hicho hakijaanzishwa hapa nchini, wanafunzi waliokuwa wakitaka kusomea masomo ya ukutubi na uhifadhi nyaraka walilazimika kwenda Makerere, Uganda.
Alisema mbali ya uwepo wa chuo hicho, changamoto kubwa inayowakabili ni ufinyu wa bajeti, uhaba wa miundombinu hasa upungufu wa mabweni na madarasa kiasi kwamba wanalazimika kuwa na shift mbili za masomo (asubuhi na jioni) hali ambayo inaathiri utoaji wa elimu chuoni hapo.
Katika risala yao, wanafunzi wanaohitimu waliomba wapatiwe ajira za moja kwa moja kama ilivyo kwa walimu au askari, pia waliomba maktaba ya chuo hicho ipanuliwe kwa sababu ni ndogo na ikiwezekana chuo kiongezewe kompyuta kwa sababu zilizopo hazitoshi wanafunzi wote kufanya mazoezi kwa vitendo.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAPILI, NOVEMBA 17, 2013

Friday, November 15, 2013

HABARI YA KIMATAIFA

RAIS DKT KIKWETE NCHINI SRI LANKA NOVEMBER 14, 2013


 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa alipomtembelea kwa mazungumzo kwenye jengo la Temple Trees jijijini Colombo leo Novemba 14, 2013 kabla ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya ya madola mwaka huu (CHOGM 2013)
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisaini  kitabu  cha  wageni nchini  sri Lanka
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa pamoja na  viongozi  mbali  mbali
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais wa Sri Lanka Mhe. Mahinda Rajapaksa katika mazungumzo yao  leo (picha  zote na Ikulu)

Thursday, November 14, 2013

MIUNDOMBINU MASHULENI SIYO RAFIKI KWA WALEMAVU




PICHA
Kashindye Kisamvu, mwanafunzi mwenye ulemavu wa miguu aliyemaliza
mtihani wa kidato cha nne katika shule ya sekondari Mwangaza mjini
Mpanda mkoani Katavi akifurahia kupata baiskeli mpya ya kutembelea
iliyotolewa na kampuni ya uwindaji ya Tanzania Big Game, mwanafunzi
huyo amelalamikia kitendo cha ukosefu wa miundombinu rafiki kwa wenye
ulemavu shuleni kwake kuwa ni kikwazo kikubwa kwa maisha yake shuleni
hapo, hali ya kukosekana kwa miundombinu duni katika taasisi hasa
shule imekuwa ikilalamikiwa na wenye ulemavu wengi hapa nchini lakini
hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa na wahusika.

Kashindye alisema kuwa alikuwa akilazimika kuomba ruhusa kati kati ya
masomo ili aendele nyumbani kujisaidia ambapo alikuwa akitumia zaidi
ya dakika 52 kwenda na kurudi nyumbani. (PICHA ZOTE NA BLOGGER)

Katavi

KAMPUNI ya uwindaji ya Tanzania Big Game Safaries Ltd  imekabidhi baiskeli ya walemavu kwa walemavu 150 walioko katika mkoa wa Katavi zenye thamani ya shilingi million 52.5 ikiwa ni mchango wao katika jamii kutokana na faida wanayopata katika shughuli za uwindaji na utalii mkoani Katavi

Akikabidhi vifaa  hivyo  kwa  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Mpanda, mwakilishi wa kampuni hiyo, Rose Bekker alisema Kampuni ya Big Game imekuwa ikitoa msaada kwa wana jamii mbali katika maeneo
wanayofanyia kazi za uwindaji kila mwaka tangu 2005 ambapo mpaka sasa kampuni hiyo imeshakabidhi baiskeli za walemavu za kisasa zipatazo elfu tatu katika maeneo mbali mbali hapa nchini

Alisema kampuni yake pia imekuwa ikiwekeza katika ujenzi wa madarasa, ujenzi wa makanisa, vifaa vya shule na misaada kwa walemavu kwa kushirikiana na asasi isiyo ya kiserikali ya Conservation Foundation
Trust Fund (CFT) ya jijini Arusha

Alisema taasisinyake inawasiliana na asasi ya Kimarekani ya Wheel Chair Foundation katika matengenezo ya baiskeli kwa ajili ya walemavu kwa gharama ya shilingi laki tatu na nusu (350,000/=)

Katika hotuba yake mgeni rasmi wa hafla hiyo fupi, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Mpanda, Enock Gwambasa alisema kuwa hivi sasa kumekuwa na tabia mbaya ya unyanyapaa kwa walemavu katika jamii hali inayosababisha baadhi ya walemavu kuishi kwa sononi kubwa

Aliwataka walemavu kujiona kuwa nao ni sehemu ya jamii na hivyo wana uwezo wa kuzalisha mali ndani ya jamii ikiwa watajengewa uwezo wa kufanya kazi hizo, wasibweteke washiriki kikamilifu katika shughuli za
kijamii kama vile kupiga vita ujangiri kwa kutoa taarifa serikalini za uwepo wa majangiri katika maeneo yao

Jumla ya walemavu 150 walikabidhiwa baiskeli zenye thamani ya shilingi laki tatu na  nusu sawa gharama yote kufikia shilingi milioni 52.5 zote zikiwa zimetolewa na Tanzania Big Game Safaries kama mrejesho wa
faida kwa jamii inayozunguka maeneo wanayofanyia kazi zake.

Katika hali ya kusikitisha Mmoja wa waliopata msaada huo ambaye amemaliza kidato cha nne mwaka huu katika shule ya Sekondari ya Mwangaza, Kashindie Kisamvu licha ya kushukuru kwa msaada huo aliiomba serikali kuangali suala la miundombinu katika maeneo ya maofisini na madarasani kwani hakuna sehemu ya mlemavu kuingia

Alisema vyoo vya shule havimfai kabisa mwanafunzi mwenye ulemavu wa viungo alipokuwa akisoma shuleni Mwangaza alipobanwa na haja alikuwa akilazimika kuomba ruhusa kwenda nyumbani kwao kwa lengo la kujisaidia na kurudi tena shuleni hali iliyokuwa ikimsababishia kupoteza muda mwingi na vipindi vya masomo

“Nilikuwa Napata shida sana shuleni kwani madarasani hakuna sehemu ya kuingia kwa baiskeli, ofisini hakuna na vyooni nako hakuna pia sehemu ya kupita mlemavu, nilikuwa nikibanwa na haja nalazimika kuomba ruhusa kwenda nyumbani kujisaidia ndipo nirudi tena shuleni, nikuwa nachelewa vipindi vingi sana na nilikuwa naathirika sana kitaaluma” alisema
Kashindie